Hashim Rungwe Akosoa kauli za Rais Magufuli Kuhusu idara ya Mahakama, asema Zinaingilia Uhuru wa Mahakama.
Mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma CHAUMA Hashim Rungwe amesema
kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt John
Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya Mahakama nchini
iliingilia uhuru wa mahakama.

Akielezea utata uliojitokeza katika hotuba hiyo Rungwe amesema hotuba
hiyo ilionekana kama kuifundisha mahakama wajibu wake jambo ambalo lina
utata katika uongozi wa kisheria lakini hata hivyo Rungwe ameielezea
hotuba hiyo kuwa itaongeza uwajibikaji katika mahakama na haki
kupatikana kwa wakati.
Wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama Alhamisi iliyopita,
Rais Magufuli aliahidi kuipatia idara ya mahakama fedha kwa ajili ya
kuendesha shuhguli za mahakama na kuitaka mahakama hiyo kuharakisha
kusikiliza kesi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi za watuhumiwa wa
kukwepa kulipa kodi.
0 comments