Lionel Messi akutwa na tatizo la figo
Mshambuliaji
wa klabu ya Barcelona Lionel Messi hakuwepo katika mazoezi siku ya
Jumatatu ili kupimwa figo yake. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina
alikosa kucheza mechi ya nusu fainali ya kilabu bingwa duniani baada ya
kupatikana na tatizo la figo,baada ya kuwa na maumivu ya tumbo
yanayosababishwa na mawe ndani ya figo.
Taarifa ya kilabu ya Barcelona imesema kuwa Messi mwenye umri wa miaka 28 atarudi katika hali yake ya kawaida siku ya jumatano.
”Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi atafanyiwa vipimo kadhaa Jumatatu na Jumanne ili kubaini hali ya tatizo hilo la figo alilopata mwezi Disemba”,ilisema.
Alicheza dakika 90 siku ya jumapili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya kilabu iliopo chini ya jedwali ya Levante.
Siku ya Jumatano ,Barcelona itaitembelea Valencia katika awamu ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Copa del Rey ambapo wanaongoza kwa jumla ya mabao 7-0.

0 comments