Mtoto wa Miaka Mitatu Abakwa Na Kunyongwa Hadi Kufa
Mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 4 Mariam Deogratius mwanafunzi wa
shule ya awali ya Makoko iliyopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma mkoani
Mara, amebakwa kisha kunyongwa hadi kufa na mtu asiyejulikana Usiku wa
kuamkia leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara kamishna msaidizi Philllip Kalang
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa Jeshi la Polisi
linafanya Msako kuhakikisha Mhalifu anapatikana.
0 comments