Shahidi wa Paul Makonda Ajichanganya kortini Kesi ya Kubenea Kumtukana Makonda..
DENIS Mujumba, Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, ambaye pia alikuwa
Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni amefura baada ya kuulizwa maswali
wakati akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya jinai inayomuhusu Saed
Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers Ltd na pia ni
Mbunge wa Jimbo la Ubungo. Anaandika Faki Sosi.
Mujumba (39) amefikwa na masaibu hayo baada ya kubanwa kwa maswali na
Peter Kibatala ambaye ni wakili wa Kubenea wakati akitoa utetezi wake
huku hakimu wa kesi hiyo kwenye Mahakama ya Mkazi Kisutu Thomas Simba
akimtaka kupaniki.
Kesi hiyo ambayo Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ndiye
mlalamikaji, ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya viongozi
hao wawili kugombana kwenye Kiwanda cha nguo cha TOOKU kilichopo
Ubungo, jijini Dar es Salaam tarehe 14 Desemba mwaka jana.
Wakili Kibatala alimuuliza Mujumba kama ni yeye ndiye aliyekutana na
baadhi askari polisi kwenye eneo la tukio na je alikuwa anawafahamu na
pia walikuwa chini ya nani? Mujumba alijibu kuwa, aliwakuta askari hao
eneo la tukio na kumuongeza kwamba, hakujua walikuwa chini ya nani.
Kibatala: Wewe ndio mwenye wajibu wa kuchunguza kesi hiyo je wewe ndio Mkuu wa Mkuu wa Idara hiyo?
Pia aliuliza kwamba siku hiyo kulikuwepo na waandishi lakini alipataje picha za video na sauti kutoka kwa waandishi wa habari?
Mujumba: Ni kweli kulikuwepo na waandishi na kwamba niliwasiliana
na waandishi hao ili wanipe ushahidi wa picha, sauti au video.
Waandishi walinijibu kuwa hawana ushahidi huo.
Kibatala: je ulikwenda na askari wangapi?
Mujumba: nilikwenda na askari wanane au tisa.
Kibatala: wataje majina
Mujumba: Ni Sajenti Peter, PC Hamis, Joachim na Doel.
Kibatala: Shahidi hajui askari wake kwani anajua jina moja tu la mwanzo na hajataja wote.
Maswali haya yalisababisha Mjumba kukunja sura na kutoa sauti ya
juu huku akitaka kubishana, Hakimu Simba alimwambia “acha kupaniki” na
kumtaka aache kubishana na wakili.
Hakimu Simba pia alimwambia Mujumba kwamba hana uwezo wa kubishana na
wakili huyo na kuwa, anachotakiwa ni kujieleza kwa kujiamini.
Wakili Kibatala kwa kutumia sheria Namba 155(a) aliiomba mahakama
kuonesha picha za ushahidi zilizokuwa zianonesha hali halisi ya tukio.
Wakili huyo aliinesha mahakama picha ambazo zilionesha kuwepo kwa askari
walioshika bunduki na kumzingira Kubena, kwenye picha hiyo Mujumba
hakuwemo.
Hapo awali Mujumba aliieleza mahakama kwamba yeye ndiye aliyemsihi
Kubenea aende naye kwenye Kituo cha Polisi Magomeni, hivyo Wakili
Kibatala aliongeza kuwa, kwa kutokuwepo kwenye picha ile Mujumba alitoa
maelezo ya uongo. Hakimu Mkazi hata hivyo, baada ya shahidi huyo kutoa
ushahidi wake, Hakimu Simba alihairisha kesi hiyo hadi tarehe 15 na 16
Aprili mwaka huu
0 comments