Home �
burudani
,
habari
,
siasa
� Udom Watuhumiwa Kutumwa na CCM Kufukuza Mwanafunzi
Unknown |
06:47:00 |
0
comments
Hali ya sintofahamu imeibuka baada ya Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom),
kumsimamisha masomo Rais wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, Victor
Byemelwa, na kudaiwa kumwandikia barua Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa, kumueleza kwamba
wamemaliza kazi aliyowatuma.
Uongozi wa chuo hicho umethibitisha kumsimamisha masomo mwanafunzi huyo lakini ukikanusha kuandika barua kwenda kwa Kimbisa.
Jana kwenye mitandao ya kijamii, barua inayodaiwa kuandikwa Februari 5,
mwaka huu na Mshauri wa Wanafunzi wa chuo hicho, Dick Manongi, ilikuwa
ikisambazwa.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba Udom/Dos/36, ilikuwa na kichwa cha
habari: "Ukamilisho wa kazi iliyopangwa kufanyika katika koleji ya
Humanities & Social Science."
Iliendelea kusema: "Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi Udom, inapenda
kukujulisha komredi Adam Kimbisa (Mwenyekiti wa CCM Dodoma,) kuwa kazi
mliotupatia katika kutekeleza mkakati wa kuiondoa serikali ya wanafunzi
wa upande wa Humanite, imekamilika kwa kijana Victor Byemelwa (aliyekuwa
Rais) kuondolewa chuoni kwa kipindi kisichojulikana.
"Napenda kukuhakikishia kuwa kwa kuwa mashtaka yametolewa na Makamu Mkuu
wa Chuo upande wa Mipango, Utawala na Fedha na yeye ndiye Mwenyekiti wa
Kamati ya Nidhamu, ni wazi kuwa kijana huyu hataweza kamwe kurudi
chuoni hivi karibuni.
Tutumie sikukuu hii ya Chama kupanga mikakati ya kuweka serikali mpya tuitakayo mapema iwezekanavyo."
Akizungumzia sakata hilo, Manongi alikanusha kuandika barua hiyo na
kudai kuwa imeghushiwa na tayari ameshatoa taarifa polisi katika kitengo
cha ufuatiliaji makosa ya kimtandao (cybercrime) ili kutafuta
aliyeighushi.
"Barua nimeiona, lakini naomba uwasiliane pia na uongozi wa chuo, mimi
nisingependa kuzungumza hilo maana hilo suala nimelipeleka kwa watu wa
Cyber Crime Dodoma, wao watatueleza hiyo barua imetoka wapi, binafsi
sijaiandika," alisema Manongi.
Kwa upande wake, Ofisa Uhusiano Udom, Beatrice Ntenga, alisema
mwanafuniz huyo alisimamishwa kutokana na kosa la kuitisha Baraza la
Shule bila kupata idhini ya Mkuu wa Chuo au Makamu Mkuu wa Chuo na
kwamba amesimamishwa kwa muda usiojulikana.
Alisema mwanafunzi huyo anatakiwa kujibu mashtaka yake kwa mujibu wa taratibu za chuo na baadaye ataitwa kamati ya nidhamu.
"Barua hiyo tumeiona ikisambaa kwenye mitandao haijatolewa na Dean of
Student, imeghushiwa maana muhuri na saini vinaonekana 'vimeskaniwa' na
kuwekwa na hata hiyo kumbukumbu namba ya barua haipo kwa Dean ukiisogeza
utagundua mapungufu mengi. Tumepeleka huko Cyber Crime
wanafuatilia,"alisema Ntenga.
Alisema barua hiyo si ya kweli bali imetengezwa ili kutafuta huruma ya
watu huku akithibitisha taarifa za barua hiyo zimewasilishwa polisi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Kimbisa, alipopigiwa simu hakupokea na
badala yake alitaka atumiwe ujumbe mfupi wa simu, baada ya kutumiwa
ujumbe wa simu yake hakujibu
Category:
burudani,
habari,
siasa
About GalleryBloggerTemplates.com:
GalleryBloggerTemplates.com is Free Blogger Templates Gallery. We provide Blogger templates for free. You can find about tutorials, blogger hacks, SEO optimization, tips and tricks here!
0 comments