Mgombea wa Urais Marekani Donald Trump Ashutumiwa Kuwa ni Tapeli...Atakiwa Kukatwa
Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani
Mitt Romney amekitaka chama chake kumkataa Donald Trump ,akimtaja
mgombea huyo aliye kifua mbele kuwa ”tapeli”.
Bwana Romney amemshtumu Bwana Trump kwa kuwachukulia raia wa Marekani
kama wajinga katika hotuba ya siri iliotolewa kwa vyombo vya habari.
Bwana Trump hatahivyo amemkejeli bwana Romney katika mtandao wa tweeter
kama mgombea aliyefeli na ambaye hafai kutoa ushari wowote kuhusu
uchaguzi.
Viongozi wakuu wa chama cha Reupblican wameshangazwa na vile bwana Trump
anavyoelekea kushinda tiketi ya chama cha Republican kwa uchaguzi huo
wa mwezi Novemba.
Inadaiwa kuwa wanachama kadhaa wa kamati ya kitaifa kuhsu usalama wa
jamii waliandika barua ya wazi wakielezea maono ya bwana Trump kama
yasio na msingi wala sera.
Bwana Trump amejiwasilisha kama muunganishi kufuatia ushindi wake katika
majimbo saba katika ile ilipotajwa kuwa jumanne maalum na hivyobasi
kuimarisha uongozi wake katika chama chake.
Romney ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa Trump anatarajiwa kutoa onyo
katika hotuba yake siku ya Alhamisi,kwamba sera za bwana Trump ni tishio
kwa chama cha Republican na taifa zaima kwa jumla.
Bwana Romney pia ataonya kuwa uteuzi wa Trump utarahisisha harakati za Bi Hillary Clinton kushinda urais nchini humo.
0 comments