Mwanamuziki Baraka Da Prince Adaiwa Kumzalisha Binti na Kumtelekeza Mtoto..Stori Nzima Ipo Hapa
Msanii wa bongo Fleva anayetamba sasa kwa kibao chake cha siwezi,Baraka
da Prince amepata kashfa ya kumzalisha binti wa miaka wa 19 aishie
Iringa aliyejitambulisha kwa jina la Candy kisha kumtelekeza mtoto
huyo.
Akiongea na redio moja binti huyo amedai mtoto wake na Baraka da Prince
ana mwezi mmoja na nusu ambapo alimzaa kwa kwa opresheni mwezi wa
Desemba mwaka Jana.baraka
Binti huyo amedai kuwa alianza mahusiano na baraka da Prince wakati
alipoenda Iringa kipindi baba yake anafanya kazi huko na badaaye
wakakubaliana aje Dar ambapo wakawa wanaishi wote mpaka binti alipopata
ujauzito na kurudi Iringa kwenda kulea ujauzito huo.
Candy akaendelea kusema kuwa baada ya yeye kurudi Iringa hakupata
matunzo yoyote kutoka Baraka da Prince hata alipojifungua.Binti anasema
kila akijaribu kumtafuta Baraka kwenye simu hudai yuko bize na mara
nyingine humtolea maneno ya kuudhi.
Candy amedai kuwa ana ushahidi wa picha kadhaa za Baraka da Prince na
mtoto na juzi tu Baraka alivyoenda kufanya show alienda kuwaona na kutoa
ahadi kibao lakini mambo yamebaki vile vile hakuna matunzo yoyote.
0 comments